Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Awanywesha sumu wanae wawili na kuwaua

Kuzaga Benjamin Ed Kamanda wa Polisi Mbeya SACP- Benjamini Kuzaga.

Sun, 10 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja aitwae Daines Mwashambo (30) Mkazi wa Kijiji cha Mashese, Mbeya Vijijini anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuua Watoto wake wawili kwa kuwanywesha sumu ya kuulia magugu shambani aina ya "Pare Force".

Polisi wamesema Daines alifanya tukio hilo akiwa nyumbani kwake lakini vifo vya Watoto hao vilitokea muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mbeya SACP- Benjamini Kuzaga amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliotokana na Daines kutuhumiwa na Serikali ya Kijiji hicho kufanya udokozi na wizi kwa kuingia katika nyumba za Watu.

Imeelezwa kuwa baada ya kuwanywesha sumu Watoto wake, Mtuhumiwa naye alikunywa sumu lakini akawaiwa kabla haijamuua ambapo kwasasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya chini ya ulinzi wa Polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live