Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani

9629 Pic+auawa TZWeb

Thu, 21 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Biharamulo. Mkazi wa Kijiji cha Nyakatuntu wilayani hapa mkoani Kagera, Esteria John (50) amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na watu wasiojulikana.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Abraham Berenatus alisema tukio hilo lilitokea Juni 18, mwaka huu.

Berenatus alisema mwanamke huyo ni mzaliwa wa kijiji cha Kiluluma kata ya Bisibo na kwamba alihamia katika kijiji hicho.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi alisema polisi wanaendelea na uchunguzi.

Diwani wa Nyakatuntu, Festo Mtatembwa aliwataka wananchi kuacha kujichukukulia sheria mkononi kama wana matatizo wafuate sheria ili kuepusha migogoro katika njia inayokubalika hata mbele za Mungu

Chanzo: mwananchi.co.tz