Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa kwa kuchomwa moto kisa kumlawiti mtoto mpaka kufa

Nyumba Ds Auawa kwa kuchomwa moto akituhumiwa kumlawiti mtoto, kusababisha kifo chake

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wenye hasira katika Kata ya Isanga, jijini Mbeya, wanadaiwa kumuua kwa kumchoma moto mtu ambaye hajafahamika jina lake, kwa tuhuma za kumlawili mtoto wa miaka mitano na kusababisha kifo chake.

Imeelezwa tukio hilo limetokea Juzi, Jumatatu Agosti 21, 2023 saa 1:45 usiku na kwamba wananchi wenye hasira wamefikia hatua hiyo kufuatia kuwepo kwa matukio kadhaa ya watoto kupotea.

Akizungumza nasi, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Igoma ''A,'' Kata ya Isanga, Damian Mwasanguti, amesema kuwa mtu huyo aliyeuawa kwa kuchomwa moto, sio mkazi wa eneo hilo, huku akilahani kitendo cha ukatili kilichofanywa, dhidi ya mtoto.

“Kama kiongozi, baada ya kupata taarifa, nililazimika kufika eneo la tukio na kumkimbiza mtoto huyo hospitali...mtuhumiwa alikuwa akishambuliwa na wananchi lakini baadaye tukapigiwa simu kuwa amepoteza maisha baada ya kuchomwa moto,” amesema.

Baba wa mtoto aliyefariki, Benjamin Mwashilindi, ameiambia Mwananchi Digital kuwa yeye anarejea nyumbani kwake toka safari kikazi Makambako, mkoani Njombe, alipigiwa simu kuwa kuna tukio la mwanaye kulawitiwa na kupoteza maisha.

“Nilikuwa nimefika eneo la mlima nyoka nililazimika kuchukua usafiri wa pikipiki ili kuwahi ambapo nilipofika nyumbani nilikuta eneo la tukio kukiwa na mabegi na ndipo nikampigia simu mwenyekiti kujua wako wapi kwa muda huo,” amesema.

Kwa upande wake mjumbe wa nyumba kumi, Hadija Binti Masudi amesema akiwa anatoka kwenye shughuli zake za kuuza nguo, alisikia kelele za wananchi wakisema mtoto analawitiwa, ndipo alipotoka na kukuta akiwa hana nguo.

Akizungumzia tukio hilo mmoja wa mashuhuda ambaye pia ni jirani na jengo (pagala) ambalo kitendo hicho kinaidaiwa kufanyika, Shadrack Isaya, amesema alipopita katika eneo hilo alihisi harufu mbaya.

“Lakini nilipojaribu kusogea nikaona kuna njemba amevua suruali na nilitafuta upenyo zaidi kuona kulikoni, nikagundua chini yake kulikuwa na kama mtoto mdogo,” amesema na kuongeza;

“Ilikuwa giza, hivyo nililazimika kuwasha tochi ya simu ili kujua ni nini kinaendelea, nilipomulika ndipo mtuhumiwa alinyanyuka na kuanza kuvaa suruali...baada ya kumhoji kulikoni kufanya kitendo hicho, ghafla kurushia ngumi kisha kukatokea purukushani,” amesema.

Amesema kuwa baada ya kuona anaelemewa alitoa kisu na kumtishia huku akimueleza atakuja kufa kizembe ndipo wananchi walipojitokeza na kuanza kumshambulia kwa kipigo.

Mwananchi ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga, kuzungumzia tukio hilo hakuweza kupatikana, hata hivyo juhudi za kumtafuta kamanda huyo bado zinaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live