Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa akituhumiwa kusafirisha mirungi

Mirungi.jpeg Begi lililohifadhiwa Mirungi

Fri, 9 Dec 2022 Chanzo: Eatv

Martin Kinasa mkazi wa mtaa wa Dkt Mohamed Shein, Kata ya Igoma jijini Mwanza, ameuawa kwa kupigwa kisha kuchomwa moto wakati akijaribu kuwatoroka watu waliokuwa wakimkimbiza kwa kutumia bodaboda kwa tuhuma za kwamba anasafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi.

Baadhi ya ndugu wa marehemu akiwemo Peter Kinasa wakizungumza Jijini Mwanza wamesema kuwa, "Ndugu yetu aliuawa na bodaboda baada ya kupata idhini kutoka kwa polisi kuwa tukamatieni huyo mtu anayekuja huko ni mwizi wa pikipiki, kwahiyo hiyo hali ndio ilisababisha ndugu yetu akatoka duniani"

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa, akizungumza kwa sharti la kutopigwa picha, amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo lililotokea Desemba Mosi mwaka huu katika kijiji cha Nyagili, Kata ya Chabula wilayani Magu.

Chanzo: Eatv