Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Athari za mafuriko Kilosa zapungua, shughuli zarejea

Kilosa Mhm.jpeg Athari za mafuriko Kilosa zapungua, shughuli zarejea

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka amesema hali katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua imeanza kutengemaa na wananchi kurejea katika shughuli zao za maendeleo.

Usiku wa kuamkia Desemba 5, 2023 maeneo ya Rudewa na Mvumi wilayani humo yaliyoathiriwa na mvua na kusababisha kifo cha mtu mmoja mwanaume (hajafahamika) wakati akijiokoa baada ya maji kuingia kwenye nyumba yake.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo, Alhamisi Desemba 7, 2023 Shaka amesema baadhi ya maeneo ambayo hayakuwa na athari kubwa wananchi wameanza kurudi katika makazi yao kama kawaida.

“Si kwamba ni mvua iliyotupa mafuriko, tulipata mvua ya kawaida isipokuwa kingo za mto Wami uliosababisha mafuriko baada ya maji yenye nguvu kutiririka. Sasa hivi hali imerudi kawaida, huku Serikali ikiendelea kufanya jitihada za kurejesha kingo za mto huo kurudi katike eneo la asili,” amesema na kuongeza;.

“Hali imetengamaa na wananchi wameanza kurudi katika maeneo yasiyokuwa na athari kubwa, lakini yale yaliyoathirika zaidi tumezuia wasirudi kwanza.”

Shaka amesema kuna timu ya tathimini inafanya kazi tangu kutoka kwa janga hilo, akisema kesho Ijumaa Desemba 8 watakamilisha kazi hiyo na kutoa taarifa. Amesema mpaka jana Jumatano nyumba 64 zilikuwa zimeathirika.

Tuna kaya kama 327 zilizopoteza makazi, lakini tunashukuru kati ya hizo wengine wameanza kurejea. Niseme hali iko vema, inaendelea kutengemaa, ” amesema Shaka.

Jumanne Desemba 5, Mkazi wa Rudewa, Hamida Hamdani aliliambia Mwananchi Digital kuwa mvua iliyonyesha ilikuwa ya kawaida, lakini maji yalikuwa mengi na kuanza kuingia kwenye makazi ya watu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live