Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atengeneza mashine ya kuchakata plastiki kuwa dizeli

60276 Pic+mifuko

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Wakati Serikali ikitangaza Juni mosi kuwa mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki, wanafunzi wawili Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Must) wametumia fursa hiyo kutengeneza mashine ya kuchakata vitu vya plastiki kwa ajili ya kuzalisha mafuta ya dizeli.

Akizungumza na Mwananchi jijini hapa katika maonyesho ya kitaifa ya kwanza ya elimu ya ufundi jana, mwanafunzi Justin Bahati alisema mafunzo wanayopatiwa chuoni yamewapa ari ya kubuni mashine hiyo.

Mashine hiyo ilitengenezwa na Bahati kwa kushirikiana na Emmanuel Mgawe kuzalisha mafuta kwa kutumia chupa za soda, chupa za maji na vitu vingine vya plastiki ambavyo vimekuwa vikichangia uharibifu wa mazingira.

Bahati alisema mashine hiyo ina uwezo wa kuchakata kilo 10 kwa saa tano na kuzalisha lita 10 za dizeli, hivyo wanatarajia kuyauza mafuta hayo kwa punguzo la asilimia 30 kwa lita.

“Tuliona ipo haja kutengeneza mashine ambayo itatumika kuchakata mifuko ya plastiki na kuzalisha mafuta, kwa sasa inatumia makaa ya mawe lakini mipango yetu ni kuiboresha iweze kutumia umeme na gesi,” alisema Bahati na kuongeza:

“Kilo moja ya mifuko na vitu vingine vya plastiki tutanunua kwa Sh500, tunatarajia kutoa ajira katika kiwanda chetu kitakapoanza uzalishaji tayari tumepeleka sampuli ya dizeli maabara.”

Pia Soma

Mwanafunzi huyo alisema wanalenga wateja ambao ni wakulima wanaoshindwa kufanya shughuli za kilimo kutokana na gharama za mafuta kwenye matrekta.

Naye mhadhiri msaidizi kitengo cha ubunifu Must, Justin Mwakatobe alisema ili mradi huo uweze kutambulishwa na kuanza uzalishaji, unahitaji Dola 150,000 za Marekani hivyo aliiomba serikali kuwaunga mkono.

“Tunaiomba Serikali itusaidie katika uwekezaji, kwani zinahitajika Dola 150,000 za Marekani katika project (mradi) nzima, sisi kama chuo hatuna uwezo lakini Serikali wana uwezo wa kutusaidia kwenye uwekezaji,” alisema Mwakatobe.

Hata hivyo, iko hatari mradi huo ukasimama kwani Serikali imepiga marufuku mifuko ya plastiki na vifaa vyake hivyo watakosa malighafi. Pia, wanaweza kukutana na suala la mikataba ya kimataifa katika uzalishaji wa mafuta.

Chanzo: mwananchi.co.tz