Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ate yazindua mafunzo kuwajengea uwezo wanawake

Tue, 26 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha Waajiri Tanzania (Ate) kimezindua awamu ya nne ya mafunzo ya kuwajenga na kuwaandaa wanawake kushika nafasi za juu za uongozi.

Mafunzo hayo ya miezi tisa yamehudhuriwa na wanawake 31 kutoka taasisi mbalimbali za binafsi na serikali.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jumanne Februari 26, 2019 Mkurugenzi wa Ate, Dk Aggrey Mlimuka amesema mafunzo hayo huwajengea wanawake uwezo wa kujieleza na kusimama kutetea jambo mbele ya umati wa watu bila woga pindi wanaposhika nafasi za juu katika bodi.

"Hii ni mara ya nne kufanyika kwa suala hili na tunashukuru kwa sababu kampuni zimeendelea kuonyesha mwamko kwa kuwalipia wanawake mbalimbali ili waweze kushiriki mafunzo haya ili waweze kujijenga," amesema.

Mhadhiri mwandamizi wa Biashara wa Chuo Kikuu cha Uongozi Mashariki na Kusini mwa Afrika (Esami), Profesa Michael Munkumba amesema ushiriki wa wanawake katika nafasi za juu huongeza chachu ya ufanyaji kazi na uzalishaji katika sehemu wanazosimamia.

"Wote ni mashahidi, angalua idara zinazoongozwa na wanawake na zile za wanaume ila tatizo mfumo dume umetutawala sana," amesema.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz