Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atakayejisaidia ufukweni kutozwa faini ya laki 3

Coco Beach Atakayejisaidia ufukweni kutozwa faini ya laki 3

Tue, 29 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa mazingira na utalii wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Peter John, amesema kwamba mtu yeyote atakayekamatwa akijisaidia haja ndogo ama kubwa katika fukwe ya bahari au fukwe ya soko la samaki Feri, atatozwa faini ya shilingi laki tatu kwa kila kosa.

Hatua hiyo imekua baada ya wavuvi katika soko la Feri kuiomba serikali kuinusuru fukwe hiyo kwa kuweka sheria kali kufuatia baadhi ya watu kujisaidia haja ndogo na hata kubwa kwenye eneo hilo.

Wakizungumza leo Novemba 29, 2022, wavuvi hao wamesema suala la mtu kujisaidia haja ndogo na kubwa katika fukwe hiyo limeonekana kama ni la kawaida hivyo serikali inapaswa kulipa uzito bila kusubiri mpaka kutokeaa madhara ya kiafya ikiwemo magonjwa ya milipuko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live