Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atakaechoma mkaa Kigamboni kuuona ‘muziki’ wake

Mkaa Pic Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo.

Sat, 3 Jun 2023 Chanzo: Mwananchi

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo amepiga marufuku uchomaji mkaa katika eneo la Pembamnazi badala yake amewataka wananchi walinde na kutunza mazingira.

Marufuku hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Nyange na Tundwi Songani ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya mtaa kwa mtaa yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea majawabu.

Mkuu wa wilaya huyo amesema kuwa serikali inahimiza utunzaji wa mazingira ambapo kwa mwaka huu imepanga kila wilaya kupanda miti million Moja na nusu ili kupambana na uharibifu wa mazingira hivyo ni wajibu wa wananchi kuendelea kutunza na kulinda mazingira ili kuendana na mabadiliko ya Tabiachi.

"Nimepata taarifa katika eneo la Kichangani na maeneo mengine wanachoma sana mkaa sasa niwaambie kwanzia sasa ni marufuku," amesema Mkuu wa wilaya huyo na nakuongeza kuwa: “Hata kauli mbiu ya Mwenge kwa mwaka huu ni tunza mazingira okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na ustawi wa taifa.”

Bulembo alisisitiza kuwa mwananchi yoyote atakayekamatwa akichoma mkaa atachukuliwa hatua kali za kisheria lengo nikukomesha tabia ya uchomaji mkaa katika maeneo yote ya Manispaa ya Kigamboni.

“Kama wilaya tumeanzisha kampeni ya upandaji miti ili kulinda mazingira na ndiyo maana katika eneo la Pembamnazi tumeshapanda miti ya mikoko 7000,” amesistiza.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi wa Manispaa ya Kigamboni kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Hassan Suluhu kutokana na uamuzi wake wa kutoa Sh.30 billion kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Kigamboni.

Chanzo: Mwananchi