Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ataka kujiua kisa Mchumba aliemsomesha amemsaliti

Kamanda Wa Polisi Mkoani Mwanza, Wilbroad Mtafungwa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mtafungwa

Tue, 7 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limesema linaendelea kufanya uchunguzi kuhusu kijana mmoja, Mwikwabe Range aliyejaribu kutaka kujiua kwa kujirusha katika kivuko cha watembea kwa miguu kilichopo Mabatini jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mtafungwa, kijana huyo alitaka kujiua kwa madai ya kumkuta mchumba wake aliyekuwa anamsomesha amezaa na mwanaume mwingine na hayupo chuoni kama walivyokubaliana.

Tukio la kijana huyo ambaye ni mwenyeji wa kijiji cha Nyamakolele kata ya Nyarero wilayani Tarime mkoani Mara, kujaribu kujiua, lilitokea Mei 3, 2024 majira ya saa 11 jioni katika kivuko hicho cha Mabatini chenye urefu wa mita 5.5 kutoka juu na kupata majeraha sehemu za usoni na mkono wake wa kulia.

Baada ya tukio hilo, kijana huyo alipelekwa katika Hospitali ya mkoa Sekeu Toure ambapo alitibiwa na baadeye kuruhusiwa. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hili ikiwa ni pamoja na kumuhoji kijana huyo na upelelezi utakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live