Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu asimulia Jenerali Msuguri alivyofunga ndoa na mmoja wa wake zake 8

90820 Umri+pic Askofu asimulia Jenerali Msuguri alivyofunga ndoa na mmoja wa wake zake 8

Sun, 5 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Butiama. Baada ya kuoa kimila na kuishi miaka kadhaa na wake zake wanane, mkuu wa majeshi mstaafu nchini Tanzania, Jenerali David Msuguri aliamua kurejea katika maisha na imani yake ya kikristo.

Akihubiri wakati wa misa ya shukrani leo Jumamosi Januari 4,2020 Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, mkoani Mara, Michael Msonganzila amesema jemedari huyo wa jeshi amerejea maisha na imani ya kikristo miaka miwili iliyopita.

"Alianza kuomba kurejea kanisani miaka minne iliyopita lakini kanisa likalazimika kutumia njia kadhaa kujiridhisha na taarifa zake za kipindi cha nyuma kabla ya kumrejesha katika huduma za kikanisa," amesema Askofu Msonganzila

"Baada ya kukamilisha taratibu kadhaa za kikanisa, Mzee Msuguri akafunga ndoa kwa kuchagua mmoja kati ya wake zake wanane."

Akufafanua, Askofu Msonganzila amesema Jenerali Msuguri alilazimika kumchagua mke mmoja kukidhi imani sharti la kanisa ya mume mmoja, mke mmoja.

"Kutokana imani ya kidini, mapenzi na mahusiano mema kati yake na wake zake, kanisa na Mzee Msuguri wamekubaliana wake zake wengine waliosalia baada ya kufunga ndoa waendelee kubaki nyumbani kwake akiwalea, kuwatunza na kuwahudumia kama wasaidizi wake yeye na mke wake," amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz