Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari wawili wadaiwa kumshushia kipigo kijana na kumsababishia kifo

Mauaji Ret Askari wawili wadaiwa kumshushia kipigo kijana na kumsababishia kifo

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: JamiiForums

Kijana aliyefariki anaitwa Mandela Petro inadaiwa alishambuliwa akiwa mtaani na Askari wawili wakimshutumiwa kuhusika katika wizi wa baiskeli ambapo baadaye baiskeli husika iliyodaiwa kuibiwa ilipatikana na kubainika marehemu hakuwa mwizi, Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.

Ikidaiwa mmoja wa Askari wanaotuhumiwa kuhusika katika tukio hilo lililotokea Juni 11, 2023 ni mwenye Namba H 3165.

Ilivyotokea Akiwa amekaa mtaani na rafiki zake Mandela Petro alivamiwa na Askari hao wawili na kuanza kumshambulia kwa kipigo huku wananchi wakishuhudia na baadhi wakirekodi kwa kutumia simu zao.

Walipoona amezidiwa na hawezi hata kuongea wakambeba na kupeleka Kituo cha Polisi Malampaka.

Wazazi wa Mandela walipopata taarifa na kufika kituoni hapo,baba na mama katika nyakati tofauti wote wakafukuzwa na Askari wakiambiwa hawana haki ya kumuona mtuhumiwa.

Baadaye mama mzazi alirejea kituoni na kuanza kuita jina la mwanaye akiwa nje karibu na madirisha ya vyumba vya watuhumiwa lakini hakukuwa na majibu kutoka kwa Mandela, ndipo Askari mmoja 'akamtonya' aende Hospitali ya Wilaya ya Maswa.

Alipofika Hospitali akazuiwa na Daktari kwa madai kuwa Mandela amechomwa sindano ya usingizi, baada ya kutumia nguvu akaingia kwenye chumba na kukuta mwanaye amefariki.

Inaelezwa ndugu walipohoji kuhusu majibu ya ‘postmortem’ ya mwili wa ndugu yao wakaambiwa Mandela alipoteza maisha kutokana na majeraha ya kichwa.

Maelezo hayo yalitolewa na Daktari anayekaa chumba namba 3 ambaye Kabila lake ni Msukuma (inadaiwa hilo lilibainika kwa kuwa alikuwa akisema yeye ndie Msukuma pekee katika kituo hicho).

Inaadaiwa Daktari huyo alijulishwa kuwa kuwa maelezo aliyopewa na Polisi ni kuwa Mandela alipigwa na Wananchi baada ya kufumaniwa, hivyo Askari walimuokoa akiwa anaendelea kupigwa. photo_2023-06-24_08-11-14.jpg Askari wanaotuhumiwa​

Msibani, Polisi wasimamia mazishi Inadaiwa Wakati wa Msiba Polisi walisimamia gharama zote za mazishi pamoja na kutoa Tsh. 200,000 kama rambirambi, kisha mwili ukazikwa Alhamis tarehe 22 Juni 2023.

Maswali ya kujiuliza Ndugu wanadai faili la ndugu yao Polisi limeandikwa kuwa kafumaniwa na kashambuliwa na Wananchi, wanahoji kama ni hivyo mbona maelezo hayaelezi ni wapi na kulikuwa na mzingira gani?

Baada ya Askari kumchukua kwanini hawakumpeleka Hospitali badala yake alipelekwa kituoni ambapo aliwekwa kwa muda kisha baadaye Hospitali?

Kama kapigwa na Wananchi, kwa nini Askari wagharamie shughuli zote za mazishi na watoe rambirambi ya Tsh. 200,000?

Inadaiwa kuwa Wananchi ambao walikuwa enep la ukio walikuwa wanarekodi kupitia simu zao kilichokuwa kikiendelea.

POLISI: Tamko la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Edith Swebe: Ajibibu madai hao yanayosambaa mitandaoni, Kamanda Edith Swebe anasema: Ni kweli Mandela Petro amefariki lakini hakuna taarifa rasmi kuwa Askari wamehusika na kifo hicho, uchunguzi wa kifo chake unaendelea pamoja na tuhuma zote ambazo zinatajwa kuhusu kilichomtokea marehemu kabla ya mauti.

Mwili wa marehemu ulifanyiwa ‘postmortem’, tunasubiri taarifa ya Daktari na kama kuna mtu yeyote anaona kuna kitu hakipo sawa aje atoe taarifa na sio kuongea mitandaoni, aje nitampokea atoe taarifa kwetu.

Tumefungua jalada tunasubiri ripoti ya Daktari na kama kuna ubishani zaidi kesi itafunguliwa Mahakamani, kinachoendelea ni tetesi.

IGP aunda tume ya uchunguzi wa mauaji ya Mandela Petro Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Salum Msangi, ameahirisha mkutano na Waandishi uliokuwa na lengo la kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa za Mauaji ya Kijana Mandela Malampaka, baada ya IGP kuunda tume ya Watu 5 kutoka Dodoma, kuchunguza tukio hilo

Kamanda Msangi ameeleza kwa sasa hawezi kulizungumza suala hilo kwa kuwa linashughulikiwa na Makao Makuu, hivyo waachwe wafanye kazi yao

Mnamo Juni 24, 2023, JamiiForums iliripoti kisa cha Mandela, anayedaiwa kuuawa na Polisi, kwa kipigo baada ya kumtuhumu kuiba baiskeli, kisha kutoa Tsh. 200,000 kugharamia msiba wake.

Chanzo: JamiiForums