Arusha. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha nchini Tanzania imewakamata askari watana akiwapo mmoja wa uhamiaji kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Frida Wikesi akizungumza na Mwananchi leo Februari 11, 2020 ofisini kwake amesema polisi hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti.
Amesema askari watatu ambao majina yao wanahifadhiwa mashauri yamefikishwa kwa mwajiri wao kabla ya kufikishwa mahakamani.
"Askari wawili mmoja wa uhamiaji Charles Mashita tayari wamefikishwa mahakamani" amesema
Amesema kuomba na kupokea rushwa ni kinyume cha kifungu cha15(1)(a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na 11 ya mwaka 2007.
"Natoa wito watu waache kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa kwani ni kosa lakini pia hata vitabu vyote vya mungu vinakataa kuomba na kupokea rushwa" amesema.
Pia Soma
- Zungu: Mifuko ya plastiki imeanza kuingia Tanzania
- Zungu asema Magufuli mgombea urais 2020, awatuliza wabunge na madiwani
- Mwakilishi kuwasilisha hoja iliyoshtukiwa na Maalim Seif