Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari wapigwa mawe na Wananchi wenye hasira, "wamevamia nyumba" RPC Kigoma (+video)

Screen Shot 2020 07 29 At 2.03.31 AM 660x400.png Askari wapigwa mawe na Wananchi wenye hasira, "wamevamia nyumba" RPC Kigoma (+video)

Wed, 29 Jul 2020 Chanzo: millardayo.com

Polisi Mkoani Kigoma wamelazimika kutumia mabomu ya machozi pamoja na kupiga risasi hewani kutawanya Wananchi wenye hasira ambao wamevamia nyumba ya mkazi wa Mtaa wa Yusuph Kata ya Mwanga Kusini, Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuharibu milango na madirisha kwa kutumia mawe.

Katika vurugu hizo wananchi wengine wamepora baadhi ya vitu ndani ya nyumba hiyo wakimhusisha mtu huyo na kupotea (kumteka ) kijana aliyetajwa kwa jina la Philipo Hussein baada ya kutoonekana kwa siku saba na inadaiwa alimchukua kijana huyo akiwa na watu wawili akisema kuwa ni Polisi wanaenda kumhoji kijana huyo katika Kituo cha Polisi.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Kigoma amesema mtu huyo anaedaiwa kumteka Philipo ni mwandishi wa habari nao wao wanalichunguza tukio.

Chanzo: millardayo.com