Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari wanne wakamatwa kwa mauaji ya kijana Geita

Semeni Hamis Locket Semeni Hamis Locket.

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: East Africa Radio

Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashikilia Askari wanne wa Uhifadhi kwa tuhuma za mauaji ya kijana Semeni Hamis Locket, mkazi wa Kata ya Nyamigota Halmashauri ya wilaya ya Geita kwa kumpiga risasi ya mkono iliyopitiliza hadi kifuani, baada ya kumkuta ndani ya hifadhi ya msitu wa Samina akichanja kuni kinyume na utaratibu.

East Africa Radio imeshiriki maziko ya kijana Semeni Hamis Locket ambapo vilio na majonzi vikiwa vimetanda miongoni mwa wanafamilia waliompoteza mpendwa wao,Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe akiwa ameambatana na watumishi wengine wa serikali wametoa pole kwa famia ya kijana huyo.

"Sijafurahishwa na sitofurahishwa na kitendo kilichofanywa na mtumishi mwenzetu wa umma ambaye alienda kujichukulia hatua za kisheria mikononi mwake kwahiyo hapa tunapozungumza watumishi wanne wa maliasili wanashikiliwa na jeshi la polisi lakini pia miongoni mwao kuna mwananchi mwingine pia ambaye alikuwa ni sehemu ya mwenzetu Semeni waliokuwa wameingia kwenye eneo hilo la hifadhi," amesema DC Geita.

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Nyamigota amesema; "Yule aliyefanya vile hakuagizwa na serikali afanye vile hata kama kijana wetu alikuwa ameingia kwenye hifadhi kimakosa lakini askari yule alitumia nguvu kubwa kwa kuwa tuna viongozi wetu hapa mkuu wa wilaya yupo hapa na taratibu nyingine zinaendelea kufanyiwa kazi kupitia vyombo vya serikali vilivyopo hapa,".

Chanzo: East Africa Radio