Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari wafariki dunia siku tatu baada ya kufunga ndoa yao

Operanews1671637767381 Askari Askari wafariki dunia siku tatu baada ya kufunga ndoa yao

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanandoa wawili ambao wamefunga ndoa Desemba 17, 2022, wamefariki dunia jana Desemba 20, kwa ajali ya gari baada ya kulivaa kwa mbele basi la kampuni ya Luwinzo lililokuwa likitokea mkoani Njombe kuelekea Dar es Salaam, katika eneo la Tanangozi mkoani Iringa.

Wanandoa hao wote walikuwa ni watumishi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, na walifariki dunia wakiwa njiani kuelekea jijini Mbeya kwenye msiba na juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa zinaendelea.

Imeelezwa pia kuwa kwenye gari walilolokuwa nalo alikuwepo mama mzazi wa mmoja wao, na kwamba alipata majeraha makubwa katika miguu yake miwili na anapatiwa matibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live