Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari polisi wafariki ajalini

68407 PIC+ASKARI

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askari watatu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani nchini Tanzania wamekufa katika ajali huku wengine wawili wakijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi la nyuma na kupinduka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Julai 26, 2019 msemaji wa polisi, David Misime amesema askari hao walikuwa wakitokea Ikwiriri kuelekea kijiji cha Mwalusembe.

Amesema ajali hiyo imetokea jana Julai 25, 2019 katika kijiji cha Kilimahewa barabara ya kilwa wilaya ya Mkuranga.

"Chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka tairi la nyuma upande wa kulia na kusababisha gari kupinduka. Askari watatu walifariki dunia na wawili walijeruhiwa akiwemo dereva. Wote wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili,” amesema Misime.

Amewataka waliofariki kuwa ni ofisa  mnadhimu Mkoa wa kipolisi Rufiji, kamishna msaidizi wa polisi Issa Bukuku; Inspekta Esteria wa ofisi ya mkuu wa upelelezi Mkoa wa Kipolisi Rufiji,  na Lameck wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Rufiji.

Amesema majeruhi ni F 7167 PC Ibrahim, aliyekuwa dereva wa gari hilo pamoja na F 7651 PC Mgusi wa ofisi ya Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz