Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari polisi mbaroni kwa rushwa ya mil 100

Masejo Kamanda Masejo

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmoja  wa askari anayetuhumiwa kuhusika na tukio la kuomba rushwa ya Sh milioni 100 kwa mfanyabiashara wa Usa River Jijini Arusha, Profesa Justine Maeda na kutoroka na ushahidi wa meno ya tembo, anashikiliwa katika kituo cha Polisi, Usa River. Anaripoti Joseph Ngilisho, Arusha…(endelea).

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Afrusha, Justine Masejo amethibitisha kukamatwa kwa Konstebo Zakhayo na kuongeza kuwa jalada la kesi hiyo linashughulikiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa.

‘’Ni kweli, Konstebo Zakhayo amekamatwa ila kesi hiyo ni ya TAKUKURU ni vema ukawauliza wanaweza kujua, sisi tumetimiza wajibu wa kukamata kwa kuwa mtuhumiwa alikuwa akitafutwa muda mrefu, baada ya kufanya tukio hilo alitoroka chini ya ulinzi wa Polisi,’’ alisema Kamanda Masejo.

Habari kutoka vyanzo vya ndani ya Polisi Usa River, zilisema Konstebo Zakhayo alikamatwa Kijenge Juu kata ya Kimandolu jijini hapa nyumbani kwa mkewe alikorudi kujificha baada ya kutokomea mafichoni kusikojulikana.

Konstebo Zakhayo na askari wenzake saba wakiwamo watano wa kituo cha Polisi Usa River na wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha na raia watatu wa Usa River, walikamatwa na taarifa ambazo gazeti la Raia mwema linazo, zinadai kuwa tukio hilo lilitokea Machi mwaka jana.

Askari waliokamatwa (majina yanahifadhiwa) ni wakaguzi wasaidizi wawili, koplo na makonstebo wanne; wawili wa kituo kikuu waliotoroka lindo na kwenda kufanya uhalifu wakiwa na silaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live