Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari magereza afariki ajali ya treni Dar

Magwreza Mkd Askari magereza afariki ajali ya treni Dar

Sun, 1 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askari wa Jeshi la Magereza, Twaibu Sultan, mwenye namba B. 4487 SGT, amepoteza maisha baada ya kutokea ajali ya basi la Jeshi la Magereza kuigonga treni ya abiria eneo la Ukonga jijini Dar es Saalam.

Ajali hiyo ilitokea jana Ijumaa Sepetemba 29,2023, ambapo mbali na kukatiza uhai wa askari huyo, pia ilijeruhi watu kumi kati yao, wanawake wakiwemo watano na wanaume watano.

Katika taarifa yake kwa umma aliyoitoa leo Jumamosi Septemba 30, 2023, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Mzee Ramadhani Nyamka alitoa pole kwa askari waliopata majeraha katika ajali hiyo, pamoja na familia ndugu jamaa wa marehemu.

Aidha Kamishna Nyamka amewataka madereva wote wa Jeshi la Magereza kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Akielezea kuhusu ajali hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk amesema ajali hiyo ilitokea jana saa 11:25 jioni baada ya basi namba MT 0040 mali ya Jeshi la Magereza kugonga treni treni ya abiria iliyokuwa ikitokea mikoa ya Bara.

“Ajali hiyo imehusisha basi la Magereza lililobeba watu 15, lililokuwa likivuka reli eneo la Kilomita 13 (Ukonga Magereza) na treni iliyobeba abiria 650 na kusababisha kifo cha mtu mmoja,” imesema taarifa hiyo na kuongeza...

Mbali na kifo pia ilijeruhi watu kumi kati yao wanawake watano na wanaume watano.

“Shirika linaendelea kuwasihi madereva wa vyombo vya moto kuwa makini wanapokatiza reli kwa kufuata sheria na alama za usalama wa reli zilizowekwa ili kuepusha ajali.

“Shirika linatoa pole kwa ndugu wa marehemu na Mwenyezi Mungu awape nafuu majeruhi ili waweze kuendelea na shughuli za kujenga taifa, taarifa zaidi zitaendelea kutolewa,” imesema taarifa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live