Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari Polisi atuhumiwa kumuua raia Arusha kwa kumpiga risasi 3

RISASI 2222222222 Askari Polisi atuhumiwa kumuua raia Arusha kwa kumpiga risasi 3

Thu, 6 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana mmoja aliejulikana kwa jina la Israel Daudi, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi 3 na askari Polisi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuachia ng'ombe kuingia shambani.

Tukio hilo limetokea katika Mtaa wa Olaresho, Kata ya Olasiti katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Akizungumzia tukio hilo Diwani wa Kata ya Olasiti, Alex Martin amesema hilo ni tukio la pili kwa askari huyo kufanya mauaji katika Kata hiyo ya Olasiti kwani huko nyuma alishafanya mauaji na Wananchi walitaka kumuua askari huyo lakini diwani aliingilia kati kwa kumuepusha askari huyo kuuliwa na Wananchi.

Lakini cha kushangaza askari huyo amerudia tena kufanya mauaji katika kata hiyohiyo.

Diwani Alex ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kutotumia nguvu na mabavu kwa raia wake pasipo sababu. Wananchi waomba sheria ichukue mkondo wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live