Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari 7 waliomwokoa mtoto ndani ya kina cha maji waandaliwa gwaride, zawadi

89755 POLIS+PI Askari 7 waliomwokoa mtoto ndani ya kina cha maji waandaliwa gwaride, zawadi

Tue, 24 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa kesho Jumanne Desemba 24, 2019 ameandaa gwaride rasmi la kuwapongeza na kuwapa zawadi askari polisi waliojitosa kwa ujasiri kwenye kina kirefu cha maji kumuokoa mtoto mwenye umri wa miaka saba aliyetaka kuzamishwa kwenye maji ya mto Morogoro na baba yake mzazi Benson Benard (31) fundi wa kuchomelea vyuma.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo Jumatatu Desemba 23, 2019 Mutafungwa amesema kazi waliyoifanya askari hao saba ni ya kujitoa muhanga kwa sababu baba huyo ambaye ni mkazi wa Kihonda Mnispaa ya Morogoro alikuwa na panga pamoja na msumeno ambaye alikuwa akiongea lugha ambazo hazieleweki.

Amesema askari hao waliofika haraka katika eneo hilo hawakuwa na maandalizi yoyote ya kukabiliana na tukio hilo na kwamba katika uokoaji huo simu, saa za askari hao ziliharibika na nyingine kwenda na maji lakini waliweza kufanikiwa kumuokoa mtoto huyo pamoja na baba yake wakiwa salama.

“Kwa kutambua ujasiri wa askari hawa mimi pamoja na maofisa wenzangu wa jeshi la polisi mkoani hapa tumeguswa na kuamua kuwapongeza vijana wetu ili kuwapa moyo.”

“Hata hivyo, tayari nimeshamuandikia taarifa mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro kuhusu tukio hilo na namna askari hawa walivyojitoa muhanga, naamini naye anaweza kuwapongeza kwa muda wake,” amesema Mutafungwa.

Kuhusu uchunguzi wa afya ya akili ya mtuhumiwa, Mutafungwa amesema leo mtuhumiwa huyo akiwa chini ya ulinzi amepelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa mwili mzima kwa ujumla.

Chanzo: mwananchi.co.tz