Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari 11 wa JWTZ waliojeruhiwa ajalini Kigoma wahamishiwa Dar

77551 Pic+askari

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Majeruhi 11 kati ya 31 ambao ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikosi cha 24 KJ katika eneo la Mnara mmoja mpakani mwa mkoa wa Kigoma na Katavi, wamepewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Ajali hiyo iliyotokea jana Alhamisi Septemba 26, 2019 ilisababisha vifo vya askari wawili wa jeshi hilo na wengine kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.

Waliofariki ni Bakari Mohammed (38) na Rashid Mwimbe (28).

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Septemba 27, 2019, ofisini kwake, mmoja wa madaktari anayehudumia majeruhi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kigoma Maweni, Lameck Mdengo amesema majeruhi 20 waliokuwa hospitalini hapo wameruhusiwa baada ya hali zao kuendelea vizuri.

"Jana mchana tulipokea majeruhi 20 na askari wawili walikuwa wamepoteza maisha, jioni tulipokea majeruhi wengine 11 ambao walikuwa katika kituo cha afya cha wilaya ya Uvinza na kufikia majeruhi 31 tuliowapokea hospitalini hapa," amesema Mdengo.

Katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma, Kaimu kamanda wa kikosi cha 24 KJ  Meja Jehuson Luhomvya amesema Septemba 25, 2019 walitakiwa kuondoka Kigoma kwenda Katavi kuungana na wenzao kwaajili ya zoezi la kusafisha misitu ya Katavi.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Amesema wakiwa njiani msafara ulifika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kilomita 20 kutoka kiwanda cha chumvi cha wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma gari moja ilipata ajali dereva aliyekuwa anaendesha gari hilo lilimshinda na kwenda kugonga mti na kuanguka kusababisha.

Amesema mpaka wakati huu majeruhi waliopo katika hali mbaya wanaowasafirisha kwenda Dar es Salaam ni 14 ambao watapelekwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam baada ya kufika hapo ndipo watajua mgonjwa yupi aende wapi na wapi.

"Askari waliobaka Kigoma hali zao zinaendelea vizuri na wataendelea kupata matibabu katika hospitali yetu ya hapa Kigoma ya kikosi cha 24 KJ na wengi tunaowapeleka Dar es Salaam kwa matibabu zaidi wamevunjika mikono na miguu," amesema Meja Luhomvya.

Hata hivyo, idadi ya majeruhi waliosafirishwa kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam inatofautiana kati ya ile iliyotolewa na daktari aliyekuwa anawahudumia na jeshi. Daktari amesema 11 huku jeshi likisema 14. Pia, daktari amesema wanapelekwa Muhimbili huku jeshi likisema wanapelekwa Lugola.

Chanzo: mwananchi.co.tz