Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asimulia alivyonusurika kifo ajali ya moto Kariakoo

Ajali Ya Moto Kariakoo Nusuriko Asimulia alivyonusurika kifo ajali ya moto Kariakoo

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: mwanachidigital

Majeruhi moto wa Kariakoo Mnadani, ambao uliharibu majengo na kuteketeza mali na bidhaa za wafanyabiashara wa eneo hilo, amesimulia alivyonusurika kifo.

Akizungumza jana Alhamisi Oktoba 5, 2023, Mohamed Hamed amesema kuwa yeye na familia yake walikuwa wanajiandaa kwenda Zanzibar lakini ghafla aliitwa na mkewe na kuambiwa kuna moto.

"Mimi na familia yangu tulikuja kwenye harusi tukitokea Uingereza na harusi ilikuwa Ijumaa iliyopita baada ya hapo tukasema tupumzike nchini mwezi mmoja lakini janga la moto limetukuta tukiwa tunajiandaa kwenda Zanzibar," amesema.

Pia Hamed amesema kelele za mkewe zilimtoa ndani akiwa amevaa bukta na kukuta moshi ukiwa umetanda sebuleni na kuwaambia watoke nje na ghafla kukawa na giza.

"Wakati nawaambia watoke nje waliniambia hawaoni ndipo nilipowafuata na kuwaambia tutafute mlango lakini kutokana na giza tukajikuta tupo kwenye choo kilichopo usawa unapotokea moto," mesema Hamed.

Hamed amesema alipogundua kuwa walipoingia ni chooni si sehemu ya kutokea aliamua kuwashika mkono na kuwapeleka chumba kingine kwa kupapasa na ndipo waipopata majereha kutokana na joto la moto huo.

Chanzo: mwanachidigital