Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asimulia alivyobaini mwanaye hasikii

Mon, 17 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kila mzazi huwa na matarajio chanya kwa mtoto anayemzaa, lakini ilikuwa ni tofauti kwa Belina Maro ambaye aliingiwa na woga alipogundua mwanaye hawezi kusikia.

Akizungumza wakati wa uwashaji wa vifaa vya kusikia (cochlear implant) kwa watoto 10 uliofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jana, Belina alisema aligundua tatizo hilo kwa mtoto wake Rehoboth Kivuyo alipokuwa na mwaka mmoja na miezi minane.

Alisema aligundua uziwi huo kwani kila alipomuita hakuwa akishtuka.

“Tulitafuta tiba bila mafanikio, baadaye tulifika idara ya masikio, kinywa na koo hapa Muhimbili walimpima na kugundua ana tatizo la usikivu, alipatiwa tiba na nashukuru Mungu leo ameweza kusikia kwa mara ya kwanza,” alisema Belina.

Daktari bingwa wa masikio, kinywa na koo, Edwin Liyombo alisema kwa takwimu zilizopo nchini kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa watatu mpaka sita wana tatizo la usikivu.



Chanzo: mwananchi.co.tz