Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 84 ya wanafunzi kidato cha kwanza hawajaripoti Biharamulo

Mwalimu Darasani 0?fit=700%2C444&ssl=1 Asilimia 84 ya wanafunzi kidato cha kwanza hawajaripoti Biharamulo

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wilaya ya Biharamulo imekuwa wilaya inayaongoza kwa asilimia 84 ya wanafunzi ambao hawajaripoti mashuleni.

Tathimini ya mwaka 2023 ina onyesha asilimia 54 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mkoani Mwanza hawajaripoti mashuleni ila asilimia 46 ya wanafunzi ndio walioripoti mashuleni.

Hivyo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa (Tamisemi) Angellah Kairuki amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuangalia sababu ya hali hiyo, ikiwa Serikali imepunguza sababu nyingi zinazochochea wanafunzi kushindwa kuripoti shule.

Waziri huyo pia amezitaja Wilaya zilizofanya vizuri kwa kuvuka asilimia 50 ya wanafunzi walioweza kuripoti shule zikiwemo, Wilaya ya Muleba, Manispaa ya Bukoba, Ngara, Kyerwa na Karagwe.

Waziri huyo amesema kuwa asilimia hiyo bado hailidhishi bado viongozi wanahitajika kujua sababu kwanini asilimia hiyo iliobaki kwanini hawajaweza ripoti.

Na ameomba kama kuna vikwazo vingine vikubwa vimewekwa na viongozi hao viondolewa na wanafunzi waripoti kwani Serikali imeweka miundombinu bora ( madarasa, madawati, umeme, maji ) inayao wawezesha wanafunzi kusoma kwa uweredi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live