Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 80 ya waandishi wa habari Tanzania hawajajiunga NSSF

69091 Pic+waandishi

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Imeelezwa kuwa asilimia 80 ya waandishi wa habari nchini Tanzania hawajajiunga na mfuko wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) jambo linalowafanya wakose mafao ya uzeeni.

Akizungumza leo Jumatano Julai 31, 2019  na waandishi wa habari jijini Mwanza katika mafunzo kuhusu NSSF marafiki, rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Deogratias Nsonkolo amesema hali hiyo huwafanya waandishi wa habari kuchangishana wenyewe wanapopatwa na matatizo.

“Waandishi wa habari wote Tanzania wapo takriban 4,500 kati ya  hao wanachama wa vilabu vyote 28 (vya UTPC) nchini ni 1,300. Tunaposema asilimia 80 ni wote wanachama na wasio wanachama,” amesema Nsokolo.

Ametumia fursa hiyo kuwataka waandishi wa habari kujiunga na mfuko huo na kuwa mabalozi wa kutoa elimu kwa jamii.

Awali mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko ameitaka UTPC kuwasaidia waandishi wa habari kujiunga na mfuko huo.

Chanzo: mwananchi.co.tz