Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ashikiliwa akidaiwa kumwagia kemikali Ofisa mtendaji

Duh Mss Ashikiliwa akidaiwa kumwagia kemikali Ofisa mtendaji

Fri, 30 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dereva wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Lusajo Makiwelu anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwamwagia kemikali watu wawili akiwemo mtalaka wake, Witness Nguvalwa (31) na mtoto wake mwenye umri wa miezi sita (jina limehifadhiwa).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, alipozungumza nasi jana Juni 29, akisema lilitokea juzi wakati mwanamke huyo na mtoto wake wakiwa wanasubiri daladala eneo la Maghorofani jijini hapa.

Amesema wamemshikilia dereva huyo kama mshukiwa baada ya mtu asiyejulikana kummwagia mtalaka wake tindikali.

"Ni kweli taarifa hizo zipo tulipata taarifa hizo na tulifanya ufuatiliaji hiyo jana( juzi) majira ya usiku na huyo mtuhumiwa tayari ametiwa mbaroni, kwa sasa tunaendelea na mahojiano" ameeleza Kamanda Martin Otieno

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Witness ambaye ni ofisa Mtendaji wa kijiji cha Idedelo mkazi Wilayani Mufindi mkoani Iringa, amesema mkasa huo ulimkuta aliposhuka kituo cha Maghorofani akitokea Mafinga Mkoani Iringa alipokuwa akisubiri usafiri wa kumpeleka atakofikia.

Amesema alikuja mkoani Dodoma kuleta wito wa Mahakama ya Mwanzo ya Mafinga kwa aliyekuwa mumewe ambaye walitenganishwa na mahakama hiyo.

"Safari yangu ilianza saa 3:00 asubuhi na gari ya Shabiby nikitokea Mafinga lengo likiwa ni kuleta wito Mahakama ya Mwanzo ya Dodoma.

"Safari ilienda vizuri hadi nilipofika kituo cha mabasi Maghorofani niliposhuka kusubiri daladala au bajaji ili niende kukabidhi wito huo,” amesema.

Amesema akiwa katika kituo hicho, alipita mwanaume mmoja ambaye hakumfahamu akiwa ameshika kichupa mkononi kilichokuwa na kimiminika na mara baada ya kumsalimia alimwagia usoni.

“Alichofanya ni kunisalimia tu dada habari na kabla sijamjibu akanimwagia tindikali. Kwa muda nilipanwa na pumzi lakini nikajitahidi nikaomba msaada kwa watu waliokuwa pembeni na kituo hicho,” amesema.

Amesema madereva bajaji na bodaboda walimsaidia na kumfikisha kituo cha polisi, ambapo alipewa PF3 na kisha walimpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambako amelazwa.

Witness amesema alikuwa akimpelekea  Makiwelu wito wa mahakama uliolenga kugawana mali walizochuma pamoja baada ya ndoa yao kuvunjwa na Mahakakama ya Mwanzo ya Mafinga mwaka juzi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Baraka Mponda amesemaa walimpokea mama huyo na mtoto wake wa miezi 6 juzi jioni waiwa wamejeruhiwa usoni kwa kumwagiwa kemikali.

Dk Mponda amesema majeruhi hao walifika wakiwa kwenye maumivu makali, mama akiwa ameathirika maeneo ya usoni, shingoni na begani na usoni kwa upande wa mtoto.

Amesema majeruhi hao wameendelea kupatiwa matibabu zaidi hospitali hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live