Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ashauri wanawake kupenda masomo ya sayansi

2dca992a596f702a3988cfe59d379f55 Ashauri wanawake kupenda masomo ya sayansi

Sun, 22 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

JAMII imehimizwa kuongeza ushawishi kwa wanafunzi wa kike kupenda masomo ya Sayansi kwa kuwa tafiti za kisayansi hususani za masula ya afya ya binadamu zinawalenga wao zaidi ya wanaume.

Mkurugenzi wa Taarifa,Teknolojia na mawasiliano ya kitafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu (NIMR) Dk Ndekya Maria Urio alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya .

Mkurugenzi huyo alikuwa anamwakilisha Mkurugenzi mkuu wa NIMR Taifa, Prof Yunus Mgaya kwenye maadhimisho ya Miaka 40 ya Taasisi hiyo.

Dk Urio alisema ni shughuli nyingi za kisayansi zinazolenga afya ya binadamu ni vigumu mwanamke kuzikwepa kutokana na mfumo wa maisha ya binadamu unaolifanya kundi hilo kuwa mstari wa mbele hata katika kunufaika na huduma za afya.

"Huwezi kuzungumzia huduma za afya ukamwacha mwanamke.Kuanzia kwenye suala la chanjo, masuala ya uzazi ,lishe, magonjwa ya milipuko, maji safi na salama, mwanamke ndiyo wa kwanza kukutana na mambo haya. Hivyo ni muhimu kwa kuwa mwanamke ndiye mlengwa wa kwanza huko mashuleni tukahimiza wao ndiyo wawe mstari wa mbele pia kupenda masomo ya sayansi."

Alipongezsa hatua ya madhimisho ya miaka 40 ya NIMR kwa tawi la Mbeya kushirikisha wanafunzi wa shule za Sekondari ikiwemo ya wasichana ya Loleza akisema ni mwanzo wa kuleta msukumo kwa wanawake kuyapenda masomo ya sayansi hasa pale wanapoona wanawake wenzao waliofanikiwa.

Kwa upande wao wanafunzi waliohudhuria maadhimisho hayo kutoka Shule ya Wavulana ya Iyunga na ya wasichana Loleza walikiri kuendelea kuwepo kwa dhana potofu kwa baadhi ya watu wanaoendelea kuamini kuwa masomo ya sayansi ni rahisi kwa mtoto wa kiume pekee kuliko wa kike jambo walilosema limepitwa na wakati.

Chanzo: habarileo.co.tz