Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ashauri mpango mkakati wa kunusuru wanafunzi 234

E635a1daf249e29ec488f366dc229ae3 Ashauri mpango mkakati wa kunusuru wanafunzi 234

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

OFISA elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi amesema ipo haja ya kuweka mpango mkakati wa kuwanusuru wanafunzi 234 wanaonekana kukosa nafasi za awali za kuingia kidato cha kwanza kwani ifikapo muda wa kuwarejesha shuleni huenda wakapotea hasa watoto wa kike.

Kahundi aliyasema hayo jana kwenye kikao cha wadau wa elimu mkoani Shinyanga wakati wa kutangaza matokeo ya darasa la saba na kusema kumekuwepo na ongezeko la asilimia 1.4 la ufaulu wa wanafunzi kwa mwaka huu.

Kahundi alizitaka halmashauri za mkoani hapa kuweka mpango mkakati wa kuwanusuru wanafunzi 234 ambao wakiendelea kukaa nyumbani wazazi watapata fursa ya kuwaozesha na wengine kuwatorosha kuchunga mifugo mikoa mingine.

“Wanafunzi 234 ndio wanakosa nafasi kati ya wanafunzi 26,382 waliofaulu mkoa mzima sawa na asilimia 78.9 kati ya hao wavulana ni 15,714 na wasichana ni 18,053 huku watahiniwa wote wakiwa 33,763 sawa na asilimia 99,” alisema.

Kahundi alisema kuwa halmashauri ya Ushetu ndiyo imeonekana kuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi wote waliofaulu huku akiwasisitiza wenyeviti wa halmashauri kuhakikisha wanaanzisha shule ili ziweze kwendana na matakwa ya idadi ya wanafunzi wanaofaulu kila mwaka.

Katibu tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela alisema kuwa mkoa umekuwa wa 17 kitaifa kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara huku shule 603 zikishiriki kufanya mtihani mwaka huu na watahiniwa wakiwa 33,767 wavulana ni 15,714 na wasichana 18,053.

Msovela alisisitiza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwani agizo la waziri mkuu ambaye alitaka ifikapo Feburuari 28, 2021 halmashauri zote nchini ziwe zimetekeleza suala hilo .

Chanzo: habarileo.co.tz