Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asakwa kwa kumuua aliyemfumania akifanya mapenzi na mkewe

DEATHSEX Asakwa kwa kumuua aliyemfumania akifanya mapenzi na mkewe.

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi mkoani Singida wanamtafuta mkazi wa Kijiji cha Ghata wilayani Singida anayetuhumiwa kuua kwa kinachodaiwa kumfumania mwanaume akifanya mapenzi na mkewe shambani.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Stella Mutabihirwa amemtaja mtuhumiwa ni Simon Mwangi (58), ambaye inadaiwa kuwa Julai 9, mwaka huu saa 11:30 alfajiri Mwangi alimuua kwa kumchoma mkuki mgongoni Innocent Dude (49) mkazi wa kijiji jirani cha Merya wilayani humo.

Kamanda Mutabihirwa amesema siku ya tukio, mke wa mtuhumiwa aliondoka nyumbani kwake saa 11 alfajiri akidai anaenda kisimani kuteka maji, ambapo amesema kwa kuwa mumewe alikuwa na fununu kuhusu uhusiano wa mkewe na Innocent alimfuata kwa nyuma mkewe bila yeye kujua.

Inadaiwa kuwa Dude aliwahi kuonywa kuhusu tabia ya kutembea na mke wa mtuhumiwa.

Kamanda Mutabihirwa amesema kabla ya kufika kisimani, mtuhumiwa alimuona mkewe akiingia shambani na yeye alipoingia humo alimkuta mkewe tayari akiwa anafanya mapenzi na Dude.

"Hapo ndipo Simon ambaye ni mtuhumiwa wa mauaji haya alimchoma Innocent mkuki mgongoni upande wa kushoto na kufa papo hapo kisha yeye kutokomea kusikojulikana," amesema na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali wa jeshi hilo unaonesha kuwa tukio hilo lilisababishwa na wivu wa mapenzi.

Kamanda Mutabihirwa amesema polisi wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa na atakapokamatwa atafikishwa mahakamani ili kujibu shitaka linalomkabili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live