Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arusha yahimizwa mgahawa wa kimataifa wa vyakula vya asili

ARUSH Arusha yahimizwa mgahawa wa kimataifa wa vyakula vya asili

Mon, 14 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafi ti na Uendelezaji wa Mboga za Asili za Majani ya World Vegetable Center ,Gabriel Rugalema amewataka wafanyabiashara Jijini Arusha kufungua migahawa yenye hadhi ya kimataifa na kuuza chakula cha asili ya kitanzania ikiwemo mboga za majani ili watalii watakapokuja kutalii nchini waweze kula chakula hicho.

Rugalema alisema hayo katika mahojiano maalumu na kusema kuwa mtalii hahitaji kula chipsi kuku wala piza kwani vyakula hivyo anakula kwao, hivyo anapokuja nchini kabla ya kwenda mbugani kutalii ama anaporudi anapaswa kula vyakula vya kitanzania ili afurahie safari yake ya kitalii.

Alisema vyakula kama mboga na matunda ni vitu adimu sana Ulaya, Asia, Amerika na mabara mengine na vikisafirishwa kutoka Afrika kwenda katika mabara hayo bidhaa hiyo hugombewa hivyo ni wajibu wa Watanzania kufungua migahawa yenye vyakula kama ugali wa muhogo,ugali wa mtama na mboga ya mchicha, sukuma.

Aliwataka wafanyabiashara kubadilika na kujikita katika biashara hiyo kwani Jiji la Arusha linasifika kwa biashara ya kitalii hivyo hawawezi kukwama iwapo watafungua mgahawa wa chakula cha asili ya mtanzania kitakachopendwa na wageni kutoka nje ya nchi.

Naye Mfanyabiashara wa mgahawa uliopo eneo la Goliondoi Jijini Arusha, Said Abdalla alisema ni wazo zuri linalopaswa kufanyiwa kazi kwani hakuna mgahawa unaouza chakula cha asili kwa ajili ya watalii Jijini Arusha.

Naye mmoja wa wajumbe wa Chama Cha Mahoteli Jijini Arusha, Karimu Mshana alisema wamelichukua wazo hilo na watakwenda kujadili ili wafanyabiashara watakaoweza kufungua migahawa ya chakula cha asili waweze kusamehewa baadhi ya vitu kwa Jiji la Arusha.

Chanzo: habarileo.co.tz