Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arusha Dc wapitisha bajeti ya Bil 57/-

Ee6d430131b5679531a9e4a5bd4e2618 Arusha Dc wapitisha bajeti ya Bil 57/-

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Arusha (Arusha DC) limepitisha bajeti ya mwaka 2021/2022 ya Sh bilioni 57 huku madiwani wakisisitiza malengo yaliyokusudiwa ya ukusanyaji mapato yavuke kwa maslahi ya halmashauri hiyo .

Katika Bajeti hiyo iliyopitishwa jana na Baraza la Halmashauri hiyo imekadiria kukusanya zaidi ya Sh bilioni 4.4 katika vyanzo vyake vya mapato ya ndani katika kipindi hicho.

Akiwasilisha bajeti hiyo Ofisa Mipango wa Halmashauri ya Arusha, Anna Urio kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Saad Mtambule alisema kuwa ruzuku ya mishahara ni Sh bilioni 40,ruzuku ya matumizi mengine bilioni 1.5 na ruzuku ya miradi ya maendeleo Sh bilioni 10.

Mtambule alisema kuwa halmashauri yake inatarajia kukusanya Sh bilioni 4.4 katika vyanzo vyake vya mapato vya ndani na bajeti hiyo ni ongezeko la Sh milioni 200 ya bajeti ya mwaka uliopita.

Alisema ukusanyaji wa mapato ya ndani, Halmashauri ya Arusha imezingatia vitu vingi muhimu na kujiridhisha katika mapato hayo hivyo mapato hayo ni ya uhalisia na hayawezi kuwaumizi wananchi wanyonge.

Mkurugenzi huyo alisema vipaumbele vya halmashauri hiyo ni pamoja na kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vitano muhimu ambazo ni pamoja na kuendeleza kitalu cha mchanga na moram katika eneo la Mirongoine,kuboresha machinjio ya Ngaramtoni kwa kukarabati mfumo wa maji taka na kujenga uzio wa machinjio ya Mirongoine na choo.

Alisema vyanzo vingine vitakavyoboreshwa zaidi ili mapato yaweze kuongezeka ni pamoja na chanzo cha mapato cha urasimishaji wa makazi katika maeneo ya Kiseriani na kujenga eneo la uwekezaji wa shughuli za vikundi na wafanyabiashara wadogo wadogo(Industrial Park).

Diwani wa Kata ya Kiranyi, John Seneu aliisifu bajeti hiyo na kuwataka madiwani wenzake kuipitisha kwani imegusa vyanzo muhimu vya ndani na vikiboreshwa kama bajeti ilivyosema halmashauri hiyo inaweza kuvuka malengo ya makusanyo tofauti na mwaka jana,

Diwani wa kata ya Olrtulot,Baraka Mollel alisema hana pingamzi na bajeti hiyo ila aliwataka watendaji na wataalamu kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa na hata kuvuka ili shughuli za maendeleo ziweze kutumika na fedha za ndani.

Baada ya kauli ya madiwani hao ndipo madiwani wote waliunga mkono na kuipitisha bajeti hiyo kwa muda mfupi kuliko miaka yote ya nyuma.

Chanzo: habarileo.co.tz