Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arejesha mtoto anayedaiwa kumuiba 2020

Mikono Mtoto Daktar Arejesha mtoto anayedaiwa kumuiba 2020

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: eatv

Baraka Masunzu (24), mzaliwa wa Kibondo mkoani Kigoma anayetuhumiwa kuiba mtoto wa bosi wake  mkoani Geita  tangu mwaka 2020 amemrudisha kwa wazazi wake baada ya miaka miwili akidai kuwa amemkuta mtoto huyo mkoani Tabora akiwa na mtu ambae hamjui  ndipo akaamua kumleta kwa wazazi

Babu wa mtoto huyo anasema mwaka 2020 kijana huyo alifika nyumbani kwake kwa ajili ya kuomba kibarua cha kulima akafanya kazi wiki chache lakini badae akatoweka na mtoto huyo.

"Alinambia ninaomba hela nikanunue nguo, nikachukua kama 20,000/=, nikamkabidhi akawa ameenda kununua nguo aliondoka na mtoto wa miaka miwili na miezi tisa, akawa ameaga anaenda kununua nguo Geita akiwa na huyo mtoto ambaye alimuiba nyumbani kwangu, basi alitoweka mpaka tulienda Polisi tukapewa RB, tukamtafuta mwisho wake ikawa tu tumekaa hivyo hivyo hatukupata jibu lolote", alisema Melki Laurent ambaye ni mzazi wa mtoto huyo

Kijana huyo alierejea na mtoto anasema baada ya kuondoka kwenye nyumba ya wazazi wa mtoto huyo alipata kazi ya kulisha Nguruwe mkoani Tabora kwa miezi sita na baada ya kazi hiyo kuisha akawa anarudi nyumbani kwako Kigoma ndipo akakutana na huyo mtoto kituo cha mabasi ndipo akamchukua kwa ajili ya kumrudisha nyumbani kwao.

Mtendaji wa mtaa wa Moringe Meshacky Katambi anasema kijana huyo alionekana mitaa ya Shilabela akiwa na mtoto huku akiwa anatafuta mahali alipomtoa ndio migambo wa mtaa huo wakamchukua kumleta ofisini na badae wakamtambua mtoto huyo.

"Nilijiridhisha wazi kwamba huyu alikuwa ameiba mtoto na Kisha mazingira yamemshinda ameamua kumleta, mwenyekiti wa mtaa alipiga simu kule Buhalahala, akawasiliana na mwenyekiti mwenzake na baadae akasema kwamba mtoto huyo, alipotea kwenye familia moja ambae mawasiliano yamefanyika na mzazi wake ndio Sasa hivi tunamsubiri", alisema Katambi.  

Chanzo: eatv