Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aporwa nyumba mbili kisa mkopo wa Milioni 5

Cd87ade8ce0221bbaaca32abfa2b794847aecc05 Aporwa nyumba mbili kisa mkopo wa Milioni 5

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga imefanikiwa kurejesha nyumba mbili zenye thamani ya Milioni 55 za Mjasiriamali, Josephine Edward Kiyuga mkazi wa Viwanja vya Mwadui Manispaa ya Shinyanga zilizokuwa zimechukuliwa isivyo halali kampuni ya kutoa mikopo.

Akitoa taarifa ya Robo ya Pili ya Mwaka wa fedha 2020-2021 (Oktoba – Desemba) Mjini Shinyanga, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Francis Luena amesema Mjasiriamali huyo ambaye anafuga kuku alikopa kiasi cha Milioni 1.5 Septemba 19, mwaka jana na kukubaliana kurejesha kiasi cha Milioni 2.1 kwa muda wa mwezi mmoja.

Luena amesema, mnamo Septemba 25, mwaka jana mjasiriamali huyo alikopa tena kwa mmiliki huyo Milioni 4 na kutakiwa kurejesha Milioni 5.6 kwa muda wa mwezi mmoja lakini mmiliki wa kampuni hiyo alimuandikisha Mkopeshwaji mkataba wa mauziano ya nyumba na siyo mkataba wa ukopeshaji wa fedha.

Hivyo, Jumla ya fedha alizokopeshwa ni Milioni 5.5 ambazo alitakiwa kurejesha jumla ya Milioni 7.7.

Hata hivyo, Mkopaji alifanikiwa kurejesha Milioni 8 kama faida ya riba ya kuchelewesha kulipa deni, lakini mkopeshaji alikataa kurejesha hati za nyumba na kudai kuwa muda wa kurejesha deni ulishapita hivyo kama mkopaji anahitaji nyumba hizo inabidi azinunue tena kutoka kwake kwa gharama ya Milioni 19 ili zitimie fedha hizo yaani Milioni 19 mkopaji alitakiwa kuongeza Milioni 11.

“Baada ya Takukuru kupata malalamiko hayo na uchunguzi kufanyika ilibaini kuwa mkopeshaji alikuwa na nia ya kujipatia nyumba hizo kwa njia isiyo sahihi, hivyo basi, TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga iliweza kuziokoa nyumba hizo na zitakabidhiwa leo (Jumatano) kwa mwananchi huyo” Luena

RAIS MAGUFULI AKIMKAMUA NG’OMBE MAZIWA

Chanzo: millardayo.com