Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apigwa na Walimu mpaka kulazwa

Mwana Mbeya Apigwa na Walimu mpaka kulazwa

Wed, 15 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Laurence Nicholaus Mwangake, Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Rohila, Mbalizi amelazwa Hospitali ya Ifisi tangu Februari 12, 2023 ikidaiwa amejeruhiwa na Walimu wanne na Walinzi wawili waliomfungia kwenye Chumba na kumuadhibu baada ya kumkamata.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ifisi, Dkt. Hamis Bakari Ally amesema “Mgonjwa ana majeraha Kichwani, Mkononi, Goti na Mguuni lakini anaendelea vizuri.

Kwa maelezo yake amekiri kudokoa Maandazi akidai alikuwa na njaa, alipoona adhabu imemzidi akaruka Dirishani na ndipo akaumia zaidi.”

Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Ernest Hinju, alipoulizwa amesema wanafanya uchunguzi na watatoa taarifa baadaye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live