Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anusurika kuuawa kwa kukatwa mapanga

Mapanga Mama Anusurika kuuawa kwa kukatwa mapanga

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ngw'anza John ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Kilugala kilichopo Kata ya Nhobora wilayani Itilima mkoani Simiyu amejeruhiwa kwa kukatwa na panga na mtu asiyejulikana maeneo ya kichwani na kwenye vidole vya mikono na kusababisha vidole viwili kukatika.

Tukio hilo limetokea nyumbani kwa mwanamke huyu ambaye alikuwa na mtoto wake mdogo ambapo hakuweza kumtambua mwanaume aliyemkata na panga.

"Tulikuwa ndani tu nilikaa nikawashiwa tochi usoni nikaanzia kupigwa mapanga ilikuwa ni saa mbili nikapiga yowe, sasa watu wakaja.

"Nilikuwa nakaa na katoto kangu kadogo sasa kalikimbia kwenda kwenye majirani kwenda kuwaambia kalikuwa kanalia sana kanapiga yowe majirani wakaja sasa kunisaidia," ameeleza Ngw'anza John ambaye ni Majeruhi aliyevamiwa.

Tayari mwanamke huyo amefikishwa hospitalini kwaajili ya kupatiwa matibabu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live