Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anusurika kufa baada ya kushambuliwa na tembo

78799 Pic+tembo

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Makoye Matondo (50), mkazi wa kijiji cha Bukore Wilaya ya Serengeti amelazwa hospitali ya Nyerere wilayani humo baada ya kujeruhiwa na tembo.

Akizungumza leo Jumatatu Oktoba 7, 2019 mganga mkuu wa hospitali hiyo, Tanu Warioba amesema Matondo alifikishwa katika hospitali hiyo jana Jumapili.

Ofisa wanyamapori wa Wilaya hiyo, John Lendoyani amesema Matondo alikuwa anatoka katika sherehe na akiwa njiani alikutana na mnyamapori huyo na kumjeruhi.

"Alijeruhiwa kwenye nyonga tumeishawataarifu hasa walioko pembezoni mwa maeneo ya hifadhi kuepuka kutembea usiku bila tahadhari maana ni kipindi ambacho tembo wanatembea sana kutafuta malisho," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz