Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anusurika kufa akiokoa godoro

Hanang Topez Anusurika kufa akiokoa godoro

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia maafa ya mafuriko yaliyosababisha kuharibika kwa nyumba na miundombinu mingine, huku wengine wakipoteza maisha kutokana na kuporomoka kwa tope na mawe kutoka katika Mlima Hanang, Katesh Mkoani Manyara, baadhi ya majeruhi katika hospitali ya Tumaini wamefunguka mazito.

Mmoja kati ya majeruhi aliyejitambulisha kwa jina la Martina anasema kuwa akiwa nyumbani kwake alishtuka kuona mafuriko ya tope yamewavamia ghafla bila ya wao kujiandaa.

Martina anaendelea kueleza kuwa alipoona mafuriko yanaanza kuingia ndani, alijaribu kuokoa vitu vyake kama vile godoro lakini baada ya kuviokoa na kujaribu kutoka nje mafuriko yalizidi na nyumba yake kubomoka na yeye kusombwa ambapo alipelekwa na mafuriko mpaka alipokutana na gogo ndipo akajiokoa kwa kulishikilia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live