Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayepumulia mashine atapeliwa bodaboda

79882 Mashine+pic

Tue, 15 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mgonjwa anayepumua kwa msaada wa mashine, Hamadi Awadh (28) amelazwa hospitalini alipata presha na kupata shida ya kupumua baada ya kutapeliwa Sh1.05 milioni.

Akizungumza na Mwananchi jana, Awadh alisema alinunua bodaboda kupitia michango mbalimbali ambayo alikuwa akitumiwa katika simu yake, ambayo baadaye alifikiria kutafuta biashara ili iendelee kumuingizia kipato.

Ofisa uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Neema Mwangomo alisema walimpokea Awadh Oktoba 2 na kumlaza kutokana na hali aliyokuwa nayo.

“Nimelazwa nina siku kumi sasa, nilipata tatizo la presha na hivyo kasi ya uhemaji ikazidi kushuka baada ya kutapeliwa,” alisema.

“Kinachonishangaza nilimuamini huyo mtu kwa sababu nilipitia Serikali za Mtaa wa Kipawa na nilimkabidhi hizo fedha mbele ya wajumbe wawili wa mtaa. Niliambiwa ningeletewa baada ya siku tatu. Hivi tunavyoongea, wiki tatu zimeisha sijui chochote na siwezi kwenda polisi kutokana na hali yangu,” alisema Awadh.

Mtendaji wa kata ya Kipawa, Rukia Masenza alisema ofisi yake haina taarifa ya tukio hilo.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Mjumbe wa serikali ya mtaa huo ambaye anadaiwa kupewa fedha hizo, hakupatikana kuzungumzia suala hilo, hata hivyo mmoja wa wajumbe aliyejitambulisha kwa jina la Habiba alisema analifahamu suala hilo na kwamba linashughulikiwa.

“Awadh alinipigia simu juzi usiku akanieleza akiwa amelazwa, lakini kwa sasa sipo ofisini niliuliza kuhusu hilo nikaambiwa linafanyiwa kazi, lakini bodaboda ipo tatizo haijabadilishwa jina kutoka kwa mtu aliyemuuzia kwenda kwenye jina lake,” alisema.

Hata hivyo, suala hilo lilipingwa na Awadh ambaye alisema tangu ametoa fedha hizo hajawahi kupewa mrejesho na alishalipia malipo yote, ikiwemo fedha za TRA ambazo wajumbe hao walimwahidi kwenda kufuatilia.

“Hili suala lina utapeli ndani yake kwa sababu wao walisema ndani ya siku mbili wangeniletea pikipiki, lakini mpaka leo hakuna chochote. Kadi ya pikipiki wameondoka nayo wenyewe, sina pikipiki wala kadi, wiki tatu sasa zimeisha,” alisema.

Awali Awadh alisema fedha hizo zilipatikana baada ya kupata msaada kutoka kwa watu mbalimbali.

“Nilifikiria kununua pikipiki ili inisaidie kuingiza kipato, na wao wajumbe waliniambia kuna mtu ana mali yake wanamjua wakaja naye kwangu wakanijazisha fomu,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz