Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila imeendelea kumfanyia vipimo mgonjwa anayepumua mashine, Hamad Awadh (28).
Baada ya kufanya vipimo vya awali Septemba 12, 2019 na kumrudisha nyumbani, gari la wagonjwa la hospitali hiyo limemfuata tena nyumbani kwake Kipawa leo Jumatatu Septemba 16, 2019 kwa ajili ya kumfanyia vipimo vingine.
Gari hilo liliwasili nyumbani kwa Awadh saa 1 asubuhi na kumchukua mpaka Mloganzila ambako anaendelea na vipimo chini ya jopo la madaktari.
“Kuna vipimo nilipimwa Alhamisi ambavyo majibu nitachukua leo lakini bado naendelea na vipimo zaidi chini ya uangalizi wa madaktari,” amesema Hamad.
Juni 10, 2019 Hospitali ya Taaluma na Tiba – Mloganzila ilimpa msaada wa mashine hiyo ya kumsaidia kupumua yenye thamani ya Sh4 milioni, kutokana na matatizo yake ya afya ambayo yanamlazimu kutumia mashine ya oksijeni muda wote ili aweze kupumua.
Awadhi alifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila Julai 9, 2018 na kuruhusiwa Juni 9, 2019 baada ya afya yake kuimarika.
Pia Soma
- Majaliwa achukizwa DC na DED kutoelewana, atoa maagizo kwa CAG,TBA
- Rais Magufuli amtaja Tundu Lissu, asema alitelekeza jimbo lake
- Upande wa utetezi wataka jitihada zaidi kukamatwa watuhumiwa watano kesi ya Mo
> VIDEO: Tanesco yatoa Sh11.5 milioni kwa mgonjwa anayepumulia mashine
> ATCL kumsafirisha bure anayepumulia mashine
> VIDEO: Anayepumulia mashine achukuliwa na gari la wagonjwa kwenda Mloganzila