Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anayedaiwa kumuua mwanae kwenye ndoo ya maji kupimwa akili

HUKUMU Anayedaiwa kumuua mwanae kwenye ndoo ya maji kupimwa akili

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Iringa limesema limeanza kuchunguza tukio la mwanamke mkazi wa Mawelewele, Manispaa ya Iringa, Johari Mbuma Twaha anayetuhumiwa kumuua mwanae kwa kumzamisha kwenye ndoo ya maji chooni ikiwamo kumpima afya ya akili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema hayo leo Jumatano Novemba 22, 2023.

"Huyu binti baba yake yuko Dar es Salaam alisema anataka kwenda huko kuhangaika na maisha na anasema huku maisha magumu yamemshinda, hivyo baba yake alimwambia aende (Dar es Salaam) bila mtoto,” amedai.

Mkurugenzi wa Shirika la Pamoja linalojihusisha na masuala ya kijamii, John Paul amesema hatua ya kumpima akili kabla ya kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo imeonyesha uungwana na haki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live