Kijana aitwaye Daudi Lufungulo (30) amepoteza maisha baada ya kuzama majini wakati akioga kwenye bwawa la maji lililopo eneo la Mtaa wa Samina, Kata ya Nyankumbu mjini Geita.
Mkuu wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji wilayani Geita, Wambura Fidelis alithibitisha tukio hilo juzi wakati akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Samina mara baada ya kuokoa mwili wa marehemu.
Wambura alisema uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha ajali hiyo ni kina kirefu na wingi wa tope wa bwawa hilo ambalo marehemu alienda kuoga na kujikuta amezama.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Samina, Joseph Kazungu alisema marehemu alikuwa ni mtu ambaye si mwenyeji sana eneo hilo kwani hana muda mrefu tangu amehamia Mtaa wa Samina.
“Ukiangalia marehemu ni mtu ambaye amekuja hivi karibuni, inawezekana hakujua kina cha hili dimbwi, amekuwa labda akiliona na kuogelea hakujua kina chake kipo vipi,” alisisitiza Kazungu.
Shuhuda wa tukio hilo, Golani Simon alisema marehemu aliwakuta eneo hilo wakiwa wanafua na aliwaomba sabuni ili aoge na alipopewa sabuni alivua nguo na kujirusha kwenye maji kisha kuzama.
Shemeji wa marehemu, Joel Daudi alisema kabla ya umauti walimualika marehemu waende kuoga naye kwenye dimbwi hilo naye aligoma na kuwaarifu hakuwa tayari kwenda kuoga muda huo.
Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera amesema timu yake ya zamani inanafasi ya kushinda dhidi ya USM Alger kama itajipanga vizuri kwa ajili ya mechi zao mbili za Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Zahera anasema Yanga ya sasa sio ile ya mwaka 2018 ambayo ilipoteza ugenini lakini ikafanikiwa kushinda nyumbani katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
“Ukiingalia Yanga iliyocheza dhidi ya USM Alger mwaka 2018 na hii ambayo itacheza Fainali, kuna mabadiliko kwa 100%. Kila mmoja anajua historia ya Yanga wakati mimi nikiwa kocha.”
“Tulifungwa na USM Alger kwao [Algeria] lakini tuliwafunga kwenye mechi ya marudiano hapa [Dar].”
“Wakati tunapoteza kule Algeria kulikuwa na kundi kubwa la wachezaji waligoma kusafiri kwa sababu za madai ya mishahara [Chirwa, Ngoma, Yondani] hatukusafiri na mshambuliaji hata mmoja!
“Tulisafiri na jumla ya wachezaji 13 tu! Kwenye benchi tulikuwa na wachezaji wawili.”
Mwaka 2018 Yanga ilikuwa kundi moja na USM Alger [Kundi D] kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, katika mechi mbili dhidi ya USM Alger, Yanga ilipoteza 4-1 ugenini [Algeria] halafu ikashinda 2-1 nyumbani [Dar, Tanzania].
#NestoShayoUPATES