Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amuua mumewe kwa kumng'ata ulimi

Mauaji WA0010 Amuua mumewe kwa kumng'ata ulimi

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Julius Rubambi (38), ambaye ni Ofisa wa Kilimo katika Kata ya Neruma wilayani Bunda mkoani Mara, amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu pamoja na kung'atwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo sehemu za siri pamoja na ulimi, na mkewe aitwaye Elizabeth Stephen (30), ambaye naye amejeruhiwa vibaya hali iliyosababishwa alazwe katika hospitali ya Kibara.

Inasemekana kuwa chanzo cha ugomvi huo ni mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa ameanzisha mahusiano mengine nje ya ndoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salim Morcase pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt.Vicent Naano, wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tayari mwanamke huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi huku uchunguzi ukiendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live