Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amtoroka mumewe akiwa mgonjwa, arejea akiwa marehemu

Vlcsnap 2022 06 09 20h46m37s092.png Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani.

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: Tanzania

Ester Mganwa mkazi wa mtaa wa Kilimahewa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, amenusurika kipigo kutoka kwa waombolezaji katika msiba wa mume wake Juma Mandoo wakimtuhumu mwanamke huyo kutenda kosa la kumtoroka marehemu mume wake akiwa mgonjwa na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine.

Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Ludewa katika mazishi ya mwanaume huyo bwana Linus Malamba ambaye pia ni kaimu katibu tawala wa wilaya ya Ludewa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

“Kilichotokea ni kwamba yule mama hakujitokeza mumewe alipofariki kwasababu alikuwa ameolewa na mtu mwingine,kwa hiyo umati wa wanawake waliona wamezalilishwa na yule mwanamke mwenzao kwa kitendo cha kutelekeza mgonjwa na mwili wa marehemu ndio maana wakaanza kumuazibu pia kwa kummwagia unga”Alisema bwana Mlamba

Hata hivyo amesema viongozi mbali mbali wakiwemo wa dini na serikali waliweza kukaa na wanawake waliotenda makosa hayo kwa mfiwa mwenye mtoto mmoja kwa kuwa aliomba radhi kutokana na makosa yake huku akitoa wito pia kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Chanzo: Tanzania