Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amchoma moto mfanyakazi wake wa ndani kwa tuhuma za kuiba sh 161,000

Polisi MszR89C.jpeg Amchoma moto mfanyakazi wake wa ndani kwa tuhuma za kuiba sh 161,000

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia Christina Shiriri kwa jina maarufu la Manka, miaka 43, mfanyabiashara na mkazi wa Usagara, Wilaya ya Misungwi kwa kosa la kumfanyia ukatili mfanyakazi wake wa ndani Grace Joseph, miaka 17, mkazi wa Kijiji cha Nyalwigo, wilaya ya Misungwi kwa kumwagia mafuta ya taa mwilini kisha kumchoma moto akimtuhumu kumwibia fedha kiasi cha Tsh. 161,000/=

Akitoa taarifa ya tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani humo Wiilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo lilitokea tarehe 4.6.2024 katika kata na tarafa ya Usagara Wilaya ya Misungwi ambapo Christina Shiriri alidai kuibiwa fedha zake alizokuwa amehilfadhi chumbani kwake na alipomuuliza binti yake wa kazi alikiri kuchukua fedha hizo na kuamua kumrejeshea.

Baada ya kurejeshewa fedha hizo Christina Shiriri aliamua kumfanyia ukatili binti huyo kwa kumchoma moto mikono yote miwili, tumboni pamoja na mapaja yake yote mawili.

Grace Joseph amepelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Musungwi kwa ajilli ya matibabu. Mtuhumia anaendelea kuhojiwa kwa kina na atafikishwa Mahakami mara baada ya upelelezi kukamilika.

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linatoa rai kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi wakati wanapowatuhumu watu wanaofanya makosa, badala yake wawafikishe kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua za kisheria, pia waendelee kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la Polisi ili ziweze kuchukuliwa hatua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live