Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amchinja mkewe na kutenganisha kichwa na kiwiliwili

Ombeni Mbeya Amchinja mkewe na kutenganisha kichwa na kiwiliwili

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simanzi na vilio vimetawala kwa wakazi wa kitongoji cha Masista kijiji cha Lusese Kata ya Igurusi baada ya Omben Kilawa mkazi wa kijiji hicho wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kumuua mke wake Happness Mwinuka kwa kumchinja na kutenganisha kichwa na Kiwiliwili.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo Machi 13, 2024 ambapo jirani amesema alisikia kelele kama watu wanagombana lakini baada ya nusu saa kukawa kimya na kuamua kupiga yowe ndipo watu walipojitokeza na polisi kufika wamelibomoa mlango wa chumbani kwao na baada ya kuingia Kilawa alikuwa ameshatekeleza mauaji kwa kumchinja mke wake na kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Bado Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha mauaji hayo ya kikatili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live