Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Almuni Azania waikumbuka shule yao, watoa msaada wa vitabu vya sayansi

82756 Pic+azania Almuni Azania waikumbuka shule yao, watoa msaada wa vitabu vya sayansi

Mon, 4 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Umoja wa wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari Azania wametoa vitabu 300 kwa ajili ya wanafunzi wa sasa wa shule hiyo.

Vitabu hivyo ni vya masomo ya sayansi na biashara vikihusisha masomo matano ambapo kila somo limetengewa vitabu 60.

Katibu wa umoja huo wa Azania Alumni 1992 Abdi Abuu amesema wametoa vitabu hivyo kupunguza changamoto ya upungufu wa vitabu vya sayansi shuleni hapo.

Amesema vitabu hivyo vyenye thamani ya Sh10 milioni vimenunuliwa kwa fedha zilizokusanywa na wanachama wa umoja huo wapatao 105.

“Hatupendezwi na kiwango cha elimu kilichopo sasa katika shule yetu, tulikuja wakatuambia changamoto zao na tumeanza kupunguza kidogo kidogo ikiwemo hili la vitabu,”

Hii ni mara ya pili kwa umoja huo kusaidia shule hiyo, Novemba mwaka jana walipeleka madawati 100. Mmoja wa wanachama wa Azania Alumni Harris Kapiga amewataka wanafunzi kutunza vitabu hivyo na kuvitumia kwa manufaa.

“Niwaombe wadogo zangu, wanangu msome, zingatieni lililowaleta shuleni, mambo mengine mtakutana nayo mkiwa wakubwa sasa hivi lililopo mbele yenu ni masomo,”

“Niwaombe mvitunze vitabu hivi maana kilichotumika ni fedha, si kwamba tumetoa kwa sababu hatuna matumizi nazo au hatuna watoto la hasha tumetoa kwa uchungu wa shule yetu tunataka msome katika mazingira bora, mfanye vizuri,” amesema Kapiga.

Mkuu wa shule hiyo Erasto Gumile ameahidi kuhakikisha vitabu hivyo vinatunzwa na kudumu kwa muda mrefu ili kuwasaidia wanafunzi watakaoendelea kujiunga na shule hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz