Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliypata ulemavu kwa sababu ya ajali za barabarani akumbusha madereva umakini

84760 Ajali+pic Aliypata ulemavu kwa sababu ya ajali za barabarani akumbusha madereva umakini

Mon, 18 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Watumiaji wa barabara nchini Tanzania wametakiwa kuwa makini wawapo barabarani vinginevyo roho za watu zitaendelea kuteketea bila sababu za msingi.

Kauli hiyo imetolewa na Keisy Kombo Jumbe katika kilele cha siku ya waathirika wa ajali za barabarani leo Jumapili Novemba 17, 2019 wakati wa uwashaji wa mishumaa na kumbukumbu ya waathirika  hao ambayo imefanyika katika ofisi za Chama Cha Wanasheria Tanzania (TLS) Jijini Dodoma.

Kombo ambaye ni mlemavu wa miguu kutokana na ajali za barabarani, amesema nyingi husababishwa na uzembe wa waendeshao vyombo vya moto.

“Madereva chonde sana, msipokuwa makini mnaweza kutufyeka wote tukabaki vilema au kuzikwa, lakini utii wenu ndiyo uhai wetu kwa sababu ajali nyingi zinakwepeka,” amesema Kombo.

Martin Mangu kutoka dawati la usalama barabarani kwa Jeshi la Polisi, amesema utii wa sheria bila shuruti ndiyo suluhisho la ajali nyingi za barabarani kwa sababu asilimia 74 ya ajali husababishwa na madereva wazembe.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano 2013/18 viliripotiwa vito 18,890 ambavyo vilitokana na ajali za barabarani.

Chanzo: mwananchi.co.tz