Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyezushisa kifo hayimaye afariki Dunia

Jeneza La Nguo Jeneza

Sun, 18 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Felister Sanga (61) Mkazi wa Kijiji cha Ipepo Wilaya ya Makete Mkoani Njombe amefariki dunia siku moja baada ya kuzushiwa kifo na Mtoto wake Ruth Sanga alipokuwa akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Consolata Ikonda Wilayani humo.

Inaelezwa kuwa Felister alipelekwa Hospitali June 10, 2023 na kutakiwa kupimwa vipimo vinavyogharimu Tsh.100,000 ili kujua ugonjwa wake lakini Mtoto wake alidai hana uwezo na hana Ndugu wa kumsaidia kupata Laki moja hivyo kuomba Mama yake aruhusiwe kurejea nae nyumbani licha ya Mgonjwa kuwa ICU.

Alipokuwa njiani alitoa taarifa kwa Ndugu kuwa Mama yake amefariki lakini alipofika nyumbani aliwazuia Watu kulia kwa kudai akiwa njiani Mama yake amefufuka, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ipepo Thadei Sanga amesema kwa kushirikiana na Ndugu baada ya kuzuiwa kulia walimchunguza Felister na kugundua alikuwa hai na hivyo kutangaza hakuna msiba.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Consolata Ikonda Sister Agnes Mlawa kwa niaba ya Hospitali amekiri kumpokea Mgonjwa huyo June 10,2023 na June 11,2023 Mtoto aliomba ruhusa kuondoka na Mgonjwa wake ambaye alikuwa akipata matibabu chini ya uangalizi maalumu (ICU).

Msemaji wa Familia, Sheritiel Sanga amesema Mgonjwa huyo hakurejeshwa tena Hospitali na alifariki June 13,2023 na kuzikwa siku hiyohiyo na hata mwili haukupelekwa tena Mochwari kwakuwa wanakiri walikosea kubaki na Mgonjwa nyumbani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live