Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyepotea siku 7 akutwa amefariki Ziwa Tanganyika

97198 Pic+chadema+kifo Mvuvi Afariki Ziwa Tanganyika

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: ITV

Mwili wa Mvuvi aliyefahamika kwa majina ya Yamungu Seif Amani aliyepotea kwa siku 7 alipokuwa akiendelea na shughuli za uvuvi Ziwa Tanganyika umekutwa kando ya ziwa hilo eneo la Burega manispaa ya Kigoma ujiji na kuzua maswali kwa baadhi ya wavuvi na wakazi wa eneo hilo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Mwenyekiti wa mtaa za Burega Samweli Mabanga wameliomba jeshi la polisi pamoja na jeshi la zimamoto na uokoaji kutoa elimu mara kwa mara juu ya namna ya kujiokoa pamoja na kuweka mawasiliano yatakayosaidia utoaji wa taarifa pindi kunapotokea ajali ziwani.

Jeshi la zimamoto na uokoaji kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Kigoma pamoja na madaktari wamefika katika eneo la tukio ambapo akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji Kilonzo Layaa amesema marehemu huyo alipotea ziwani siku ya Jumatatu ya wiki iliyopita na kwamba baada ya kupatikana kwa mwili taratibu zote zikiwemo za uchunguzi zimefanyika na mwili umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya hatua za maziko.

Chanzo: ITV